pmbet

Simba kuanza utaratibu wa kuwapima kilevi wachezaji

Eric Buyanza

July 10, 2024
Share :

Klabu ya Simba itaanza utaratibu wa kuwapima kilevi wachezaji wake wote watakaokuwa wanaingia kambini.

Habari za ndani kabisa kutoka katika kikao kilichofanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na mabosi wa klabu hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji, pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilijadili nidhamu kwa wachezaji.

Chanzo kinasema wachezaji wa timu hiyo walitangaziwa kuwa meneja mpya wa timu atakabidhiwa kifaa maalum kinachoweza kupima kama mchezaji ataingia kambini akiwa amelewa na kama itakuwa hivyo basi atazuiliwa kuingia kambini.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet