pmbet

Simba kukipiga na wababe wa Yanga sSimba Day 2024.

Joyce Shedrack

July 21, 2024
Share :

Klabu ya Simba huwenda ikacheza na klabu ya APR kutoka nchini Rwanda kwenye mchezo wa kirafiki katika kilele cha wiki ya Simba Day itakayofanyika tarehe 3 mwezi wa nane 2024 kwenye dimba la Benjamini Mkapa. 

Uongozi wa klabu ya Simba ulituma barua kwa timu tatu tofauti ikiwemo Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Apr, na Sekhukhune United ya Afrika Kusini kuzialika kushiriki katika sikukuu hiyo  na mpaka sasa timu ambayo tayari imeonyesha nia kuitikia wito wa mnyama ni mabingwa hao wa Ligi Kuu Nchini Rwanda.

 

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni tarehe 5 january 2024 kwenye michuano ya mapindukizi cup hatua ya makundi mchezo uliotamatika kwa sare ya bila kufunguna.

 

Hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya mapinduzi cup iliwakutanisha  Yanga na APR Fc tarehe 7 January 2024 wananchi wakiambulia kipigo cha goli 3-1.

 

Msimu uliopita klabu ya Simba ilicheza na Power Dynamos ya Zambia kwenye tamasha la Simba Day na kupata ushindi wa goli 2-0.

 

Unadhani hiki kitakuwa kipimo sahihi kwa mnyama ?.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet