Simba kupimana nguvu na timu ya daraja la pili Misri.
Joyce Shedrack
July 21, 2024
Share :
Klabu ya Simba imetangaza kucheza mchezo wa kirafiki kwa mara ya kwanza tangu ianze maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao Nchini Misri (Pre season) mchezo utakaopigwa siku ya kesho jumatatu majira ya saa 11:30 jioni nchini Misri.
Kikosi cha Mnyama kilichosheheni wachezaji wengi vijana waliosajiliwa msimu huu kitashuka dimbani kupimana nguvu dhidi ya El-Qanah inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Misri.