Simba kushuka dimbani leo tena dhidi ya timu ya Saudia
Sisti Herman
July 29, 2024
Share :
Klabu ya Simba leo itacheza mchezo wa tatu wa kirafiki kwenye maandalizi yao ya msimu mpya yanayoendelea nchini Misri dhidi ya klabu ya Al-Adalah ya ligi daraja la kwanza nchini Saudi Arabia kwenye dimba la Suez Canal kuanzia saa moja kamili usiku.
Huo unakuwa mchezo wa 3 wa Simba kwenye 'Pre Season' baada ya kushinda 3-0 dhidi ya Canal SC na ushindi wa jana wa 2-1 dhidi ya Telecom Egypt.