Simba kushusha Winga hatari kutoka Zambia.
Joyce Shedrack
June 13, 2024
Share :
Klabu ya Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na mchezaji wa Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu Nchini Zambia Joshua Mutale mwenye umri wa miaka 22 raia wa Zambia.
Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya winga ya kulia amefunga magoli 8 na kutoa pasi za mwisho za magoli (assist) 7 kwenye Ligi Kuu Nchini humo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinasema mshauri wa mwekezaji wa Simba Moo Dewji, Crescentius Magori anayetajwa kuwa kwenye kamati ya Usajili wa Simba msimu huu yupo Nchini Zambia kuzinasa saini za wachezaji kadhaa waliopo kwenye rada za Simba.