Simba kuwakosa Kapombe na Kagoma leo Fountain Gates.
Joyce Shedrack
April 15, 2026
Share :
Klabu ya Simba inatarajia kushuka dimbani leo majira ya saa 10 jioni kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gates FC huku wakiwakosa nyota wao wawili wa kikosi cha kwanza kutokana na kazi 3 za njano walizozipata kwenye michezo iliyopita.
Wachezaji hao ni beki wa kulia na nahodha wa msimbazi Shomari Kapombe na kiungo Yusuph Kagoma ambao kocha Steven Barker amethibitisha kuwa hawatakuwa sehemu ya kikosi cha mchezo huo.

"Timu yetu itawakosa Kagoma na Kapombe kwenye mchezo wetu wa kesho, ni wachezaji muhimu wenye uzoefu wa kiimataifa, ni pigo kuwakosa lakini kama ambavyo mara zote nawaambia kuwa huwezi kushindania ubingwa kwa kuwategemea wachezaji 11 pekee ni lazima ihusishe wachezaji wote ulionao," amesema Barker.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo Aprili 15, 2026 katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha, ambapo Fountain Gate FC watakuwa wenyeji wa Simba.





