Simba kuwavaa Dodoma jiji leo
Sisti Herman
May 17, 2024
Share :
Klabu ya Simba leo itashuka dimbani kuvaana na Dodoma jiji kwenye dimba la Jamhuri Dodoma, kuanzia saa 10 jioni kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Simba iliyopo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikihitaji kushinda mechi zake ili kumaliza kwenye nafasi 2 za juu kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika.
Dodoma jiji waliopo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wanahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka pazuri kuepuka kushuka daraja.