"Simba lipeni kwanza kisasi cha Yanga ndo mje kwetu" - Kocha Jwaneg'
Sisti Herman
March 1, 2024
Share :
Kocha wa Jwaneng' Galaxy Morena Cuthbert Ramoreboli amesema anawashangaa klabu ya Simba kuuchukulia mchezo dhidi yao kuwa wa kisasi cha misimu mitatu iliyopita huku wakisahau kulipa kisasi cha goli 5 walizofungwa na Yanga mwaka uliopita.
"Nawashangaa Simba wametangaza kufanya kisasi na sisi Jwaneng kwanini wasifanye kisasi cha kufungwa mabao 5 Kwanza waliyofungwa hapa, Sisi hatufahamu mambo ya kisasi na badala yake tumekuja kutafuta matokeo," alisema kocha huyo.
Simba watawakaribisha Jwaneng' kesho jioni kwenye dimba la mkapa kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kundi B huku kila upoande ukiwa na nafasi ya kuweza kufuzu.