Simba na Azam kushiriki Muungano Cup Zenji
Sisti Herman
April 21, 2024
Share :
Shirikisho la soka Zanzibar (ZFF) na Shirikisho la soka Tanzania Bara (TFF) kwa pamoja wamethibitisha kurejea tena kwa michuano ya kombe la Muungano baada ya miaka 20 kupita bila kuchezwa.
ZFF na TFF katika urejeo huo wa kombe la Muungano wamevialika klabu za Simba na Azam kwa upande wa Tanzania Bara na Mabingwa ligi kuu Zanzibar msimu huu KMKM pamoja na klabu ya KVZ kwa upande wa Tanzania visiwani.
Michuano itaanza April 23 kwenye uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.