Simba na Azam, nani bingwa leo fainali ya Muungano Cup
Sisti Herman
April 27, 2024
Share :
Katika kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, leo utachezwa mchezo wa fainali ya kombe kla Muungano kati ya klabu ya Simba dhidi ya klabu ya Azam kwenye dimba la New Aman Complex Zanzibar kuanzia saa 2 usiku.
Michuano hiyo ambayo imerejeshwa baada ya miaka zaidi ya 20, ilizikutanisha timu 4 kutoka pande mbili za Muungano. mbili kutoka bara na mbili kutoka visiwani huku timu za visiwani KMKM na KVZ vikiondolewa na timu za bara, Simba na Azam.
Simba waliwaondoa KVZ kwa goli 2-0 kisha Azam wakawaondoa KMKM kwa goli 5-2.