Simba na Ismaily vitani kumgombea Josephat Bada
Eric Buyanza
July 2, 2024
Share :
Simba wameamua kurudi tena nchini Ivory Coast, na taarifa zikufikie kuwa mabosi wa klabu hiyo wako kwenye maongezi ya kumsajili kiungo mkabaji Arthur Josephat Bada, kutoka ASEC Mimosas.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Simba wamekutana na hali ya sintofahamu baada ya klabu ya Ismaily ya Misri kuweka dau zito mezani kwa ajili ya kuinasa saini ya mchezaji huyo.