Simba na JKT waanza walipoishia, Fountain wakibanwa WPL
Sisti Herman
April 15, 2024
Share :
Ligi kuu ya wanawake Soka Tanzania Bara Serengeti Lite imerejea hii leo kwa michezo ya mzunguko wa pili kuendelea huku vinara Simba Queens wakiendelea walipoishia baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa sifuri ugenini dhidi ya Ceasiaa Queens mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Samora Mkoani Iringa, goli pekee la mchezo huo likifungwa na Aisha Juma.
Timu nyingine zilizoshuka dimbani Leo ni JKT Queens wakiwakaribisha Bunda Queens mchezo uliotamatika kwa JKT kupata ushindi wa goli 2-1.
GeitaGold Queens walicheza na Alliance Girls mchezo uliomalizika kwa sare ya goli 2-2 .
Mchezo mwingine ulizikutanisha Amani Queens dhidi ya Fountain Gates kwenye dimba la shule ya Nyangao ambapo uliisha kwa sare ya kutokufungana.