pmbet

Simba na KVZ kwenye ufufuko wa Muungano Cup leo

Sisti Herman

April 24, 2024
Share :

Baada ya kufufuliwa upya baada ya miaka 20, michuano ya Kombe la Muungano leo inatarajiwa kuanza ambapo kutakuwa na mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya Simba na Kikosi cha Valentia Zanzibar (KVZ) utakaochezwa majira ya saa 2 usiku kwenye dimba la New Amani Complex.

Simba wenye mfululizo mbaya wa matokeo kwenye ligi kuu Tanzania bara ambapo hawajashinda mcozo hata mmoja kwenye michezo mitano iliyopita huku wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wanaenda kukutana na KVZ ambao wapo nafasi ya 4 kwenye ligi kuu Zanzibar.

KVZ wana nyota kama Abdul-aziz Makame 'Bui' aliyewahi kucheza Yanga, Polisi Tanzania na Namungo pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Singida Big Stars, DTB, Mbeya City, Gwambina na Mbeya kwanza Chunga Said ambaye amejiunga nayo dirisha la mwezi Januari na hadi sasa ameshatikisa nyavu za ligi hiyo mara 2 kabla ya kusimama.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet