pmbet

Simba na Singida BS kukiwasha leo CECAFA Kagame Cup.

Joyce Shedrack

July 25, 2026
Share :

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kagame Cup Simba na Singida Black Stars leo zitaanza kutupa karata yao ya kwanza ya kuwania ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) 2026 katika mechi zao za kwanza jijini Kigali Rwanda.

Simba na  Singida Black Stars zitacheza kwenye uwanja wa Pele kwa muda tofauti wakianza Chui wa Singida kuivaa Jamus FC ya Sudan Kusini  saa 10:00 jioni kabla ya Mnyama Simba kucheza dhidi ya Magadishu City ya Somalia saa 1 usiku.

Singida inaingia kwenye michuano hiyo ikiwa ni mabingwa watetezi, baada ya kutwaa taji hilo mwaka jana huku Simba ikirejea kwenye michuano hiyo baada ya kukosa kushiriki katika matoleo manne mfululizo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet