pmbet

"Simba na Yanga wameniheshimisha" - Karia

Eric Buyanza

March 6, 2024
Share :

Rais wa TFF, Wallace Karia, amezipa kongole klabu za Simba na Yanga kwa kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisema wameipa sifa nchi, na pia wamemuheshimisha yeye mbele ya viongozi wa mashirikisho mengine ya soka Afrika na dunia.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo, timu za Simba na Yanga zimetinga kwa pamoja hatua ya robo fainali huku Tanzania ikiwa nchi pekee iliyoingiza timu mbili katika hatua hiyo.

Mara nyingi imezoeleka kuona nchi za Kaskazini maarufu nchi za Kiarabu hususan Misri, Morocco na Tunisia zikiingiza timu mbili katika hatua hiyo, lakini safari hii ni Tanzania pekee iliyofanikiwa kufanya hivyo. 

"Nazipongeza Klabu za Simba na Yanga, kuanzia viongozi na wachezaji wao, kuingia kwao hatua ya robo fainali kumeiheshimisha nchini yetu, ni Tanzania pekee iliyoingiza timu mbili msimu huu, wameniheshimisha mimi kama Rais wa TFF mbele ya viongozi wenzangu na Mashirikisho ya Soka Afrika na duniani kwa jumla.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet