Simba na Yanga zitakutana nusu fainali - Rage
Sisti Herman
December 21, 2023
Share :
Aliyekuwa mwenyekiti wa wa klabu ya Simba na mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage ametabiri uwezekano mkubwa wa Simba na Yanga kukutana kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa baada ya kushinda michezo yao ya raundi ya 4 ya hatua ya makundi na kufanikiwa kufikisha alama 5 wote kwa pamoja.
“Yanga imeshinda, hii ni furaha kwa watanzania wote, mimi na bashiri kuna uwezekano kwenye nusu fainali wakakutana Yanga na Simba kulingana na misimamo ya makundi yao, bado wana nafasi ya kuvuka” Rage aliiambia PMTV baada ya mchezo kati ya Yanga na Medeama.
Mahojiano haya utayapata kwenye mtandao wa Youtube wa PMTV.
Yanga walishinda mchezo wao dhidi ya Medeama kwa magoli 3-0.