"Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kuhitaji huduma ya Maxi Nzengeli.
Joyce Shedrack
August 28, 2026
Share :
Kiungo wa Yanga Maxi Mpia Nzengeli amefunguka kuwa klabu ya Simba ndiyo iliyokuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kuonyesha nia ya dhati na kutuma ofa rasmi ya kumhitaji kutoka AS Maniema Union.

Akizungumza kupitia podcast ya The Physics ya Denis Nkane Maxi ameweka wazi kuwa ingawa Simba ilitangulia mazungumzo na taratibu zao hazikufika pazuri hali iliyotoa fursa kwa Yanga kuingilia kati na kufanikisha dili.
Maxi amefafanua kuwa dili lake la kwenda Yanga lilirahisishwa zaidi na mahusiano mazuri na ya karibu ya kibiashara yaliyokuwepo kati ya bosi wa AS Maniema Union, Jenerali Amisi Kumba, na uongozi wa Yanga.
Ushirikiano huo ulikuwa umeimarika kufuatia mafanikio ya usajili wa wachezaji waliotangulia kufanya vizuri kutoka DRC kama Fiston Mayele na Tuisila Kisinda.





