pmbet

Simba ni mali ya umma, haiwezi kuchukuliwa kinyemela tu - Kigwangala

Eric Buyanza

June 13, 2024
Share :

Iko hivi; tatizo lilianzia kwenye mfumo wa uwekezaji. Hatukupaswa kuwa na mwekezaji mmoja tu, walipaswa kuwa wasiopungua watatu na wasiozidi watano.

Mwekezaji mmoja amejikuta ‘demi god’, amefika mahali anaona kuwa hii timu ni mali yake peke yake - anajipa umungu-mtu sasa.
 

Wakati kwa mujibu wa hizo MEMARTS anazoamini zinampa mamlaka (ambazo kimsingi siyo halali maana hajalipia hisa zake) kwa kuwa ana hisa 49% tu. Hana haki ya kisheria ya kufanya maamuzi peke yake, kwa kuwa yeye ni mwanahisa mdogo (minority shareholder), wanachama ndiyo wanahisa wakubwa (majority shareholders) maana tuna hisa nyingi zaidi, 51%, na tuna mamlaka makubwa zaidi ya kufanya maamuzi kisheria.
 

Wanachama ndiyo wenye haki na mamlaka kubwa zaidi ya kufanya maamuzi ndani ya Simba. Aidha, kuhusiana na uendeshaji wa club wa kila siku, Bodi ya wakurugenzi ndiyo chombo cha juu zaidi cha maamuzi kwa niaba ya wote (wanachama na mwekezaji).
 

Shida iliyopo sasa, mchakato umetupa wanachama nguvu ya hisa 51% lakini umempa mwekezaji Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa wanachama amebaki kuwa muhuri tu ama boya.
 

Najibu hoja dhaifu za chawa na vibaraka wa Glezabhai kama ifuatavyo:
 

1. Hana mamlaka ya kufanya chochote ndani ya Simba sababu hajalipia hisa.

2. Anachojaribu kufanya ni kuleta chaos kwenye club. Wanaosema ‘Yeye’ kumaanisha washampa mamlaka ya kumiliki timu kama yake ni mbumbumbu wa sheria na taratibu hivyo wapuuzwe.

3. “Hataki ujinga kwenye usajili msimu ujao! Kwamba, atasajili wachezaji ‘yeye mwenyewe’, kwani yeye ni nani? Hii ni kauli ya kuwatomasa watu wasiojielewa. Kama anaitakia mema Simba asimamie club iweke mifumo ya good governance, siyo yeye kuleta chaos kwa kuunda mfumo wake binafsi pembeni.

4. Glezabhai anaweza kumtaka yeyote yule awe mjumbe wake ama aondoke, ni haki yake, lakini awe ndani ya utaratibu siyo nje ya utaratibu. Taarifa zilizopo ni kwamba hao wajumbe wake kwenye bodi wamekataa kupitisha mapendekezo ya madai yake kuwa anaidai Simba zaidi ya bilioni 20, hivyo akilipa na zile bilioni 20 zitakuja kuwa bilioni 40, basi na  timu itakuwa ya kwake 100% (kwa mujibu wa thamani kamili ya club).

Maana mhasibu wake alitaka Bodi ipitishe kuwa hayo madeni “anayoidai” Simba yawe capitalized (yawe mtaji wake), wakakataa; wakamdai alete mikataba ya hiyo mikopo na matumizi ya hizo pesa akashindwa - kurudisha taarifa kwa Glezabhai, tajiri akanuna. Kwa kuwa hata wajumbe aliowateua kulinda maslahi yake kwenye Bodi walikataa, akiwemo Jaribu Tena, akaamua kuwatimua.

Sasa kuua soo, kaamua kuunda kamati yake na kudai kusimamia usajili ‘yeye mwenyewe’!

5. Glezabhai hataki Mkurugenzi wa wanachama, hataki Mkurugenzi wa Benchi la ufundi wawepo, ila anataka asimamie usajili yeye binafsi na washkaji zake tena nje ya utaratibu!

Kumbukeni: lengo la kufanya transformation lilikuwa kuondoa huu ujanja ujanja na kuleta corporate governance iliyonyooka. Tumefikia lengo?

6. Binafsi, sina shida na Glezabhai kuinunua Simba, hata kama iwe 100%, bado ntaishabikia tu, lakini afuate utaratibu. Siyo kutugeuza watu wote wajinga.

7. Ili kuondoa haya matatizo ya ujanja ujanja na kuweza kufikia kuwa na timu yenye corporate governance nzuri ni lazima kusiwe na mwekezaji mmoja pekee - wawe watatu na wasizidi watano! Hata kama watapatikana kwa fedha kidogo kabisa, lakini mifumo ikiwekwa vizuri Simba itafanya vizuri tu.

Simba ina potential ya kuingiza zaidi ya bilioni 20 kwa mwaka mmoja tu, kitu gani bilioni 20 ya Glezabhai?

8. Wanasimba wengi ni kama samaki tu, wanatamani kusema tatizo maji yamewajaa mdomoni. Kuna wale wanaoamini Glezabhai akisusa tutashuka daraja, wengi tumezaliwa tumeikuta Simba na hakukuwa na Glezabhai na Simba iliweka rekodi zake. Ikawa Gleza anajitoa na Simba ikashuka daraja, akili zitakuja; maana ukitaka kwenda peponi lazima ufe!
 

Wanasimba na watanzania kwa ujumla tuondoe fikra za kimaskini. It’s pathetic!
#HK #Fighter #NjeYaBox

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet