"Simba ni timu kubwa hata bila mimi" Chama.
Joyce Shedrack
August 20, 2025
Share :
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba raia wa Zambia Clatous Chota Chama amejibu ujumbe wa mwanasoka kwenye ukurasa wake wa instagram kuhusu picha mjongeo alizozichapisha akiwa anafanya mazoezi na binti yake nyumbani kwake.

Mwanamichezo huyo maarufu aliandika “Dah ungekuwa zako Misri sasa hivi ila ukawasikiliza walimwengu”Chama amkajibu huku akimwambia Simba ni timu kubwa hata bila uwepo wake.
"Maisha yanaendelea na sote tunapaswa kuendelea. Klabu ya Simba ni timu kubwa iwepo na mimi au bila mimi, nilitimiza wajibu wangu nilipokuwa kwenye klabu. Sasa ni wakati wa wale waliopo moja kwa moja ndani ya klabu kusukuma mbele na kufanya vizuri zaidi. Tuko pamoja sana 🙌🏿🙌🏿🙌🏿" Majibu ya Mwamba wa Lusaka aiyetikisa msimbazi kabla ya kutimkia Jangwani kwa msimu mmoja.





