Simba Queens kubeba Ubingwa leo Mwanza
Sisti Herman
June 7, 2024
Share :
Endapo watashinda mchezo wao wa leo kwenye ligi kuu wanawake dhidi ya Alliance Girls, klabu ya Simba Queens leo watatawazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo wakiwa na michezo mitatu mkononi.
Simba Queens kwasasa wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na alama 43 baada ya michezo 14 ya ligi hiyo na endapo wakishinda mchezo wa leo watafikisha alama 46 ambazo haziwezi kufikiwa na washindani wao kwenye michezo mitatu iliyobaki.
Washindani wa Simba Queens ni JKT Queens waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 34 ambao nao wana mchezo dhidi ya Yanga Princess iliyopo nafasi ya tatu, mchezo utakaochezwa kesho kwenye dimba la Mej. Jen. Isamuhyo
Je Alliance wataweza kuwazuia Simba Queens kuwa Mabingwa?