Simba Queens kutangaza rasmi ubingwa wa ligi siku ya kesho.
Joyce Shedrack
May 26, 2026
Share :
Klabu ya Wanawake ya Simba Queens siku ya kesho inatarajia kutangaza ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake Tanzania bara endapo watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya Tausiwakiwa ugenini kwenye uwanja wa KMC Complex.

Simba Queens ambao ni mabingwa mara nne wa ligi ya wanawake wanahitaji alama 3 tu katika michezo 4 iliyosalia ili kurejesha rasmi taji la ligi mitaa ta Msimbazi wakiwa na alama 52 kileleni mwa msimamo wakiwa tofauti kwa alama 10 na wapinzani wao wawili JKT Queens na Yanga Princess.
2017 - Mlandizi Queens
2017/2018 - JKT Queens
2018/2019 - JKT Queens
2019/2020 - Simba Queens
2020/2021 - Simba Queens
2021/2022 - Simba Queens
2022/2023 - JKT Queens
2023/2024 - Simba Queens
2024/2025 - JKT Queens
Mpaka Sasa Simba Queens na JKT Queens ndio wamebeba Mara nyingi Zaidi Ubingwa wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania Simba Queens Mara 4
JKT Queens Mara 4 na Mlandizi Queens Mara 1.





