pmbet

Simba Queens kutangaza Ubingwa leo Chamazi

Sisti Herman

May 9, 2024
Share :

Endapo watashinda mchezo wao wa leo kwenye ligi kuu wananwake dhidi ya Bunda Queens, klabu ya Simba Queens leo watatawazwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo wakiwa na michezo mitatu mkononi.

Simba Queens kwasasa wawapo kileleni mwa msimamo wakiwa na alama 40 baada ya michezo 14 ya ligi hiyo na endapo wakishinda mchezo wa leo watafikisha alama 43 ambazo haziwezi kufikiwa na washindani wao kwenye michezo mitatu iliyobaki.

Washindani wa Simba Queens ni JKT Queens waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 31 ambao nao wana mchezo dhidi ya Yanga Princess iliyopo nafasi ya tatu, mchezo utakaochezwa kesho kwenye dimba la Mej. Jen. Isamuhyo

Je Bunda wataweza kuwazuia Simba Queens kuwa Mabingwa?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet