Simba Queens njia nyeupe Ligi ya Mabingwa Afrika
Sisti Herman
July 24, 2024
Share :
Mabingwa ligi kuu wanawake Tanzania Simba Queens msimu wa 2023/24 ambao pia ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa wamepangwa kundi B kwenye michuano ya kuwania kufuzu ligi ya Mabingwa Afrika ukanda wa Afrka Mashariki na Kati (CECAFA).
Simba wamepangwa kundi B na klabu kutoka mataifa mengine kama PVP Buyenzi (Burundi), Kawempe Ladies (Uganda) na FAD Djibouti (Djibouti).
Kundi lingine ni kundi A lenye timu za CBE (Ethiopia), Kenya Police Bullets (Kenya), Yei Joints (Sudan Kusini), Warriors Queens (Zanzibar) pamoja na Rayon Sports (Rwanda).
Mashindano hayo kwa msimu huu yatafanyika nchini Ethiopia.