Simba Queens yalifata kombe Ethiopia bila Aisha Mnunka.
Joyce Shedrack
August 14, 2024
Share :
Kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Soka ya wanawake Tanzania bara Simba Queens kimeanza safari ya kwenda nchini Ethiopia kwaajili ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa)itakayoanza Agosti 17 hadi Septemba 4, 2024 nchini humo.
Michuano hiyo ambayo pia ilishawahi kufanyika Tanzania bingwa atakata tiketi ya kushiriki fainali za Klabu Bingwa Afrika (CAFWCL)ambazo Simba ilishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2022 na kuishia hatua ya nusu fainali huku msimu uliopita JKT Queens waliiwakilisha Tanzania na kuishia hatua ya makundi.
Simba Queens imepangwa Kundi B ikiwa pamoja na PVP Buyenzi ya Burundi, Kawempe Muslim Ladies ya Uganda na FAD ya Djibouti na itashuka dimbani kwa mara ya kwanza tarehe 18 dhidi ya FAD ya Djibouti.
Kikosi cha timu hiyo kimeondoka Nchini na wachezaji 24 pasipo mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake Aisha Mnunka ambaye bado ni mchezaji wa klabu hiyo lakini hajawahi kuripoti kambini tangu kikosi hiko kianze maandalizi ya mashindano hayo.