Simba Queens yamsaini Amina wa Yanga kutoka JKT Queens
Sisti Herman
July 25, 2024
Share :
Klabu ya Simba Queens imekamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Yanga na mchezaji bora wa ligi kuu wanawake Tanzania na COSAFA 2022 Amina Ally Bilal kutokea JKT Queens kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Amina anaungana na nyota wenzake waliokuwa nao Yanga Princess misimu miwili nyuma kama Marry Saiki Atunike, Precious Christopher na Wincate Kaari.
Simba Queens ipo kambini kujiandaa na michuano ya kimataifa ambapo itaanza na michezo ya kuwania kufuzu ligi ya Mabingwa Afrika ukanda wa CECAFA ikiwa kundi B na timu za PVP Buyenzi, Kawempe Ladies na FAD Djibouti.