Simba Queens yashusha mshambuliaji kutoka Ethiopia.
Joyce Shedrack
July 27, 2026
Share :
Klabu ya Simba Queens imemtambulisha mshambuliaji wake mpya raia wa Ethiopia Senaf Demise.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa kwenye rada za Simba tangu misimu miwili iliyopita hatimaye wamefanikiwa kupata saini yake akitokea CBE ya Ethiopia.
Senaf anatarajiwa kuitumikia rasmi Simba Queens kuanzia michuano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika nchini Rwanda.





