Simba wakija kulipa kisasi litakuwa kosa kubwa sana.
Joyce Shedrack
April 19, 2024
Share :
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Garmondi kwenye press kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby utakaopigwa kesho katika dimba la Benjamin Mkapa amewaambia Simba waingie uwanjani kucheza mpira na sio kulipa kisasi .
“Wanapaswa kuja kucheza ili washinde mechi na sio kulipa kisasi, kama wanakuja kulipa kisasi litakuwa kosa kubwa sana, timu inapaswa kucheza ili ishinde pekee na sio kisasi”
Mashabiki wana haki ya kutamani mabao mengi lakini ni ngumu kurejea kilichotokea mechi iliyopita kwangu ni muhimu zaidi kuweka ari ya ushindi kwa wachezaji wangu."
Sambamba na hayo Gamondi pia amemzungumzia Kocha Mkuu wa klabu ya Simba na kusema anajua itakuwa mechi ngumu
"Namfahamu sana Benchika ni rafiki yangu wa muda mrefu najua hawezi kuingia kwenye mtego wa hisia za mashabiki na itakuwa ni mechi nyingine mpya ngumu kwa kila upande."