Simba wamsajili beki wa Aziz Ki Burkina Faso
Sisti Herman
July 7, 2024
Share :
Klabu ya Simba imethibitisha kumsajili beki wa kushoto raia wa Burkina Faso Valentin Nouma kutoka klabu ya St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Nouma mwenye umri wa miaka 24 pia ni mchezaji wa timu ya Taifa Burkina Faso ana uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja lakini pia ni mtaalamu wa mipira iliyokufa.
Nouma anatarajiwa kusaidiana na beki wa kushoto na nahodha wa Simba Sc, Mohammed Hussein, Zimbwe Jr kwenye nafasi hiyo.