Simba washusha beki kutoka Sauzi
Sisti Herman
July 4, 2024
Share :
Klabu ya Simba imekamilisha uhamisho wa beki wa kati wa kimataifa wa Tanzania Abdulrazak Hamza kutoka klabu ya Supersports United ya nchini Afrika kusini kwa mkataba wa miaka miwili.
Hamza mwenye umri wa miaka 21 pia aliwahi kucheza Namungo, Mbeya City na KMC kwa nyakati tofauti kabla ya kutimkia Afrika kusini.
Hamza pia ni mchezaji wa timu ya Taifa na ametumikia timu za vijana za taifa.