Simba watafanikiwa kufikia mataji ya Yanga Muungano cup?.
Joyce Shedrack
April 27, 2026
Share :
Baada ya kufanikiwa kufuzu fainali ya Muungano Cup klabu ya Simba ipo kwenye nafasi ya kumfikia mtani wake kwenye idadi ya Mataji ya michuano hiyo waliyokusanya mpaka sasa.

Klabu ya Yanga imetwaa mataji mengi zaidi ya Muungano ikiwa ina mataji 7 wakati Simba wakiwa wana mataji 6 hivyo endapo Simba watafanikiwa kubeba kombe hilo tarehe 29 basi atafikia idadi sawa na Yanga huku Yanga pia ikiwa kwenye nafasi ya kutanua utawala wake kwenye Michuano hiyo.
Orodha ya Mabingwa wa muda wote wa Muungano Cup tangu 1982:
1. Young Africans SC (7) — 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000, 2025
2. Simba SC (6) — 1993, 1994, 1995, 2001, 2002, 2024
3. Majimaji FC (3) — 1985, 1986, 1998
4. Malindi FC (2) — 1989, 1992
5. KMKM SC (1) — 1984
6. Tanzania Prisons SC (1) — 1999
7. African Sports Club (1) — 1988
8. Pan African SC (1) — 1982
Kuanzia mwaka 2003, mashindano yalisimama baada ya Yanga kugomea kushiriki, wakieleza kutoridhishwa na mfumo wa mashindano. Hali hiyo ilisababisha kusimama kwa mashindano kuanzia 2004 hadi 2024 yaliporudi tena.
Nani atakuwa bingwa wa 2026? ![]()





