Simba ya Benchika ni ushindi na burudani
Eric Buyanza
December 15, 2023
Share :
Klabu ya Simba leo imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Kagera Sugar huku mashabiki wakishiba na burudani ya soka safi chini ya kocha Abdelhak Benchika.
Mabao ya Simba yamefungwa na Saido Ntibanzokiza kwa mkwaju wa penalti mwishoni mwa kipindi Cha kwanza, Sadio Kanoute aliyemalizia kwa kichwa Krosi ya Mohamed Hussein huku John Bocco akipigilia msumari wa mwisho baada ya kucheza na alama za nyakati na makosa ya mlinzi wa Kagera wakati akirudisha mpira kwa mlinda lango wake.
Simba sasa inapanda hadi nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 5 huku ikiwa na michezo mitatu mkononi.