pmbet

Simba ya msimu ujao ni moto kote kote yaifanyia umafia Yanga.

Joyce Shedrack

July 29, 2024
Share :

Klabu ya Simba Queens imethibisha kukamilisha usajili wa kiungo wa zamani wa Yanga na mchezaji bora wa ligi kuu wanawake Tanzania na COSAFA mwaka 2022 Amina Ally Bilal akitokea JKT Queens.

Hii inakuwa si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuiwakilisha nembo ya mnyama kwani msimu wa 2019/20 aliwahi kuichezea Simba kwa msimu mmoja kabla ya kutimkia Yanga alikodumu kwa misimu mitatu na baadae kutimkia  JKT Queens.

 

Kiungo huyo ambaye alikuwa kwenye mawindo ya Yanga ili arejee klabuni hapo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja msimbazi baada ya kuridhika na ofa aliyokuwa amewekewa mezani.

 

Simba Queens tayari ipo kambini kujiandaa na michuano ya kimataifa ambapo itaanza na michezo ya kuwania kufuzu ligi ya Mabingwa Afrika ukanda wa CECAFA iliyopangwa kundi B na timu za PVP Buyenzi, Kawempe Ladies na FAD Djibouti.

 

 

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet