Simba yaandika historia kuzindua Simba Day Ngorongoro.
Joyce Shedrack
August 1, 2026
Share :
Klabu ya Simba imezindua rasmi wiki ya Simba ndani ya hifadhi ya Ngorongoro ikiambatana na sherehe za kumbukizi ya miaka 90 ya klabu yao.

“Baada ya kupata wazo la kuja kufanya uzinduzi wa Wiki ya Simba tukawafikishia wenzetu wa Ngorongoro tukiwa na wasiwasi wanaweza wasikubali sababu humu hifadhi kuna sheria na miongozo yake na ili kufanya tukio kama hili unalazimika kuzivunja ili kufanikisha jambo hilo. Kwenye kikao cha kwanza na wao watafanya kila kinachowezekana bila kuvunja kanuni za kiutalii ili jambo hili lifanikiwe.”





