pmbet

Simba yaangukia pua sakata la Damaro.

Joyce Shedrack

April 2, 2026
Share :

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetupa shauri la klabu ya Simba kuhusu uhalali wa mchezaji Mohamed Damaro Camara.
Mohamed Damaro Camara ametambulishwa Yanga SC

Simba iliwasilisha malalamiko mbele ya Kamati hiyo ikipinga uhalali wa usajili wa Camara, kwa madai unaifanya Yanga kuwa na wachezaji 13 wa kigeni badala ya 12.
 

Klabu hiyo ilidai usajili wake umekiuka Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu pamoja na Kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
 

Kamati katika uamuzi wake, ilisema usajili wa Camara hauna dosari kwa vile habanwi na Kanuni zilizowasilishwa na klabu ya Simba.
 

Uamuzi kamili wa shauri hilo utatumwa kwa Mlalamikaji ambaye ni klabu ya Simba

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet