Simba yaanzisha kampeni ya kulifikisha goli la Chama FIFA.
Joyce Shedrack
May 7, 2026
Share :
Klabu ya Simba imetangaza kuanzisha kampeni ya kusambaza goli la kiungo wao Clatous Chama alilolifunga siku ya Jumapili dhidi ya Watani wao Yanga ili lifike kwenye Shirikisho la soka Duniani FIFA na lifanikiwe kuingia kwenye orodha ya kushindani tuzo ya goli bora Duniani.

Kupitia ukurasa rasmi wa klabu hiyo Simba wamechapisha video ya bao hilo huku wakiambatanisha na ujumbe kwenda kwa mashabiki wao kuwa walichapishe kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na kutag ukurasa rasmi wa FIFA.
“Dunia imeona bao bora zaidi mwaka huu ni kutoka kwa Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama. Utamu wa bao hili zaidi ni kumfunga mtani na kuchangia mtu kuliwa kichwa”.
“Jambo la kufanya kwa Mwanasimba ni kuweka post hii kwenye IG Story na kutag akaunti ya @fifa ujumbe uwafikie mapemaaaaa!!!”Wameandika klabu ya Simba.
Unaliona goli hili likishinda tuzo hiyo?.





