Simba yahamishia majeshi kwa nyota wa Nigeria
Eric Buyanza
July 12, 2024
Share :
Klabu ya Simba ipo kwenye mazungumzo na nyota raia wa Nigeria, Jonathan Alukwu , ni baada ya Mnyama kuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyo anayekipiga kwenye klabu ya Sporting Lagos.
Hata hivyo inaelezwa kuwa nyota huyo anapewa kipaumbele ili aende kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ikiwa mbio za kuipata sani ya mkongo Elie Mpanzu zitashindikana.