Simba yaikanyaga Yanga kuvuna mapato mengi uwanjani.
Joyce Shedrack
July 17, 2024
Share :
Klabu ya Simba imeongoza kwa kuingiza mapato mengi kwenye kiwanja cha nyumbani katika michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu uliopita ikiiacha klabu ya Yanga iliyoshika nafasi ya pili pili kwa kuingiza milioni 825,065,000 wakati Simba ikiingiza milioni 835,805,000 kupitia takwimu zilizotolewa na Ligi Kuu.
Licha ya klabu ya Yanga kuongoza kwa kwa kuuza tiketi nyingi kwenye michezo ya nyumbani msimu uliopita na Simba kushika nafasi ya pili kwa uuzaji wa tiketi bado Simba imevuna fedha nyingi zaidi ya timu yoyote kwenye mapato ya uuzwaji wa tiketi.
Tabora United na Mashujaa Fc ni miongoni mwa timu zilizoingiza fedha nyingi nyuki wa Tabora wakikamata nafasi ya tatu na nafasi ya nne ikiwa ni Mashujaa FC.
Klabu ya Azam imeshika nafasi ya 9 katika orodha hiyo ya timu zilizoiingiza mapato mengi zaidi kwenye Ligi Kuu msimu uliopita