Simba yajificha Zanzibar kuwawinda Al Ahly
Sisti Herman
March 18, 2024
Share :
Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amethibitisha kuwa kuanzia kesho klabu hiyo itaweka kambi ya siku 7 visiwani Unguja kwaajili ya kujiandaa kucheza mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ambao utacheza machi 29 jijini Dar es Salaam.