pmbet

Simba Yakanusha kuachana na Anicet Oura na Libasse Gueye.

Joyce Shedrack

July 22, 2026
Share :

Klabu ya Simba imekanusha taarifa zinazosambaa kuwa ipo hatua za mwisho kumuuza viungo wake washambuliaji Anicet Oura na Libase Gueye katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally ameweka wazi kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa nyota hao bado wana mkataba na ni sehemu muhimu ya mipango ya timu kuelekea msimu mpya wa mashindano.

"Kumekuwa na maneno mengi kwamba Libasse anauzwa Oura anauzwa au Loemba anaondoka lakini nikiwa hapa nikiwa nimevaa suti ya bei ghali nawatangazia kwamba hakuna mchezaji hata mmoja ambaye anaondoka. 

 

"Yoyote bora ambaye unamfahamu bado ataendelea kuwepo na leo kuna habari njema ya Selemani Mwalimu kuendelea kusalia Simba Sports Club."- Semaji Ahmed Ally.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet