Simba yamchomoa kiungo ligi kuu Nchini Tunisia.
Joyce Shedrack
July 22, 2025
Share :
Klabu ya Simba inaripotiwa kukamilisha usajili wa kiungo Alassane Kante mwenye wa miaka 24 raia wa Senegal akitokea klabu ya CA Bizertin inayoshiriki ligi kuu Nchini Tunisia.

Kiungo huyo mkabaji mwenye uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati anatarajia kucheza mchezo wa mwisho wa kuagwa siku ya leo katika klabu yake kabla ya kuanza safari ya kuja Tanzania kuanza maisha mapya na wekundu wa msimbazi.
Kante ambaye mkataba wake na CA Bizertin ulikuwa unamalizika June 30,2026 msimu uliopita alicheza mechi 25 za ligi kuu Nchini Tunisia na kufunga goli 1 pekee huku akipata kadi za njano 6.