pmbet

Simba yamtambulisha kocha na wasaidizi wake kutoka Sauzi

Sisti Herman

July 5, 2024
Share :

Klabu ya Simba Sc imemtangaza Fadlu Davids raia wa Afrika kusini mwenye umri wa miaka 43 kuwa kocha wao mkuu akichukua mikoba ya Abdelhak Benchikha aliyeondoka kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita.

Fadlu ametambulishwa Simba sambamba na wasaidizi wake ambao ni;

• ⁠Darian Wilken, kocha msaidizi
• ⁠Mueez Kajee, Mtathmini wa viwango
• ⁠Riedoh Berdien, Kocha wa viungo
• Wayne Sandilands, Kocha wa makipa

Msimu uliopita kocha huyo alihudumu kwenye kikosi cha Raja Casablanca kama kocha msaidizi chini ya kocha mkuu Josef Zinnbauer Raia wa Germany,huku wakiisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Fadlu amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet