pmbet

Simba, Yanga hapatoshi leo Chamazi

Sisti Herman

January 3, 2024
Share :

Mabingwa mara tatu wa ligi kuu wanawake (TWPL) Simba Queens leo wanawaalika watani zao Yanga Princess kwenye mchezo wa raundi ya 3 ya ligi hiyo utakaochezwa dimba la Azam Complex, Chamazi majira ya saa 10 za jioni.

 

Haya ni makala maalumu kwaajili ya mchezo huu wa watani wa jadi “Kariakoo Derby”

 

Historia fupi baina yao (Historical Background)

 

Tangu msimu wa 2019 hizi ni rekodi zilizokusanywa;

 

  • - Kukutana mara 12
  • - Simba imeshinda mara 7
  • - Yanga imeshinda mara 1
  • - Sare 4

 

Mchezaji mwandamizi wa Simba Queens Mwanahamisi Omary ndiye kinara wa mabao kwenye derby ya Kariakoo akifunga mara 10 huku akiwa ndiye mchezaji pekee aliyewahi kufunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja “hat-trick”

 

Uwezo wa sasa (current form)

 

Simba na Yanga wote kwa pamoja msimu huu wameshacheza michezo miwili ya ligi kuu wanawake, hizi hapa takwimu zao;

 

Simba Queens

 

  • - Michezo 2
  • - Kushinda 2
  • - Magoli ya kufunga 10
  • - Magoli ya kufungwa 2
  • - Alama 6
  • - Nafasi kwenye msimamo 1

 

Yanga Princess

 

  • - Michezo 2
  • - Kushinda 2
  • - Magoli ya kufunga 8
  • - Magoli ya kufungwa 1
  • - Alama 6
  • - Nafasi kwenye msimamo 2

 

Wasemavyo makocha

 

“Tumejiandaa kupata alama 3, wao pia wamejiandaa kupata alama 3, wakingia kwenye mfumo magoli yatapatikana, mipango yetu itabakia kwenye timu lakini tukianza kutaja tutakua tunatoa silaha kwa wapinzani lakini nikuhakikishie kuwa Simba imejipanga kurudisha heshima yake kwasababu ilikua mabingwa mara 3 na ikakosa mara ya 4” alisema Mussa Hassan “Mgosi”, kocha msaidizi wa Simba Queens iliyopo chini ya kocha Juma Mgunda.

 

“Kila mechi huwa ni tofauti kwahiyo hatuwezi kutarajia mambo sawa na uliyoyaona kwenye mchezo uliopita na huu ni mchezo mpya na lakini tulicheza nao kwenye ngao ya jamii na niliwaona wachezaji wao kwa kina na nikapata tarifa zakutosha kuhusu wanavyocheza” alisema kocha mkuu wa Yanga Princess Charles Haalubono.

 

Wasemavyo nahodha wa pande zote

 

“Wachezaji wamejiandaa vizuri kwaajili ya mchezo ili tuweze kutimiza malengo yetu tuliyojipangia na kuitetea Simba yetu, mchezo utakuwa mgumu kwasababu timu zote zimejiandaa vizuri kiufundi na kimbinu hivyo utakuwa wa ushindani kwahiyo tunaomba mashabiki na wapenzi wa mpira waje kuona burudani” alisema Violeth Nicholaus,  nahodha wa Simba Queens.

 

“Tumefanya kazi kubwa kwaajili ya mchezo huu na tumejiandaa kama tulivyoelekezwa na kocha wetu hivyo nadhani mchezo utakuwa mrahisi kwetu” alisema Saiki Atunike, nahodha wa Yanga Princess.

 

Je ni Simba ama Yanga? nyasi za Azam Complex zitajuta.

 

Takwimu na Rekodi ( @matukiomuhimu Instagram )

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet