Simba, Yanga kuanza na kitonga kombe la FA
Sisti Herman
January 29, 2024
Share :
Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) itaendelea Jumanne Januari 30 na mashabiki wa Simba na Yanga wataanza kuziona timu zao zikichuana uwanjani dhidi ya timu za madaraja ya chini baada ya mapumziko ya takriban mwezi mmoja kupisha michuano ya Afcon 2023.
Yanga watacheza na Hausing ya Njombe kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam saa 1:00 usiku, watani zao Simba watavaana na Tembo fc siku ya Januari 31 majira ya jioni uwanja ukiwa haujawekwa bayana huku tetesi ambazo zikisema Simba wameomba kutumia uwanja wa New Amaan Complex.
Mchezo mwingine ni kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Nyakagwe katika Uwanja wa Manungu, Morogoro saa 10:00 jioni huku ya Kagera Sugar dhidi ya Dar City kupigwa Januari 31 uwanja wa Kaitaba, Kagera.