pmbet

Simba, Yanga na Azam wakimbia Kagame Cup kisa ratiba

Sisti Herman

June 20, 2024
Share :

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya klabu za Tanzania bara zimethibitisha kuwa klabu za Simba, Yanga na Azam zote zimeandika barua kwa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) kutoshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati (Kagame Cup) kwasababu ua ugumu wa ratiba kwaajili ya msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa.

Wakati huohuo klabu ya Singida Black Stars wamethibitisha kuomba kushiriki michuano hiyo iliyopangwa kufanyika katikati ya likizo ndefu ya msimu mpya wa ligi za mataifa mbalimbali.

Michuano ya CECAFA Kagame Cup imepangwa kufanyika kuanzia Julai 6-22 visiwani Zanzibar ikihusisha timu vigogo mbalimbali kutoka ukanda huu kama Simba, Yanga na Azam huku zikialikwa timu kubwa kutoka nje ya ukanda huu kama TP Mazembe, Nyasa Big Bullet na Red Arrows.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet