Simba, Yanga zakabidhiwa timu toka Kilimanjaro
Joyce Shedrack
February 2, 2024
Share :
Droo ya kombe la Shirikisho la Azam Sport Federation Cup raundi ya 16 imefanyika hii leo huku timu zilizofuzu raundi hiyo zikimjua mshindani wa kwenda kucheza naye hatua inayofuata, vigogo wa soka la Tanzania Simba sc na Yanga SC zimepangiwa kukutana na timu za Mkoa wa Kilimanjaro.
Simba sc amepangwa na bingwa wa Mkoa huo TRA Kilimanjaro FC na bingwa mtetezi wa kombe hilo Young Africans SC imepangwa kucheza na Polisi Tanzania, Azam FC itakutana na Green Worriors .
Timu zingine zitakazo kutana hatua hii baada ya kuchezwa kwa michezo ya hatua ya 32 bora ni :
Singida FG vs FGA Talents,
Tabora United VS Nyamongo FC,
Mtibwa Sugar VS Stand United
Ihefu SC VS Mbuni FC
JKT Tanzania VS TMA FC
Kagera Sugar VS Pamba FC
Rhino Rangers VS Mabao FC
Geita Gold VS Mbeya City
Namungo VS Transit Camp
Dodoma Jiji VS Biashara UTD
Coastal Union VS Mbeya Kwanza
KMC VS Gunners
Mashujaa FC VS Mkwajuni FC.
Michezo hiyo imepangwa kucheza kati ya Februari 19 na 20 mwaka huu kwa mujibu wa Kalenda.
Mshindi wa michezo hiyo atakuwa amekata ticket ya kuingia robo fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi ni Yanga SC aliyechukua kombe msimu jana katika fainali iliyowakutanisha na matajiri wa Chamazi Azam FC wananchi walichukua kombe hilo kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Azam FC.