Simba, Yanga zatunukiwa tuzo kusaidia matibabu ya Figo
Sisti Herman
February 15, 2024
Share :
Klabu kongwe na kubwa zaidi za mpira wa miguu nchini, Yanga na Simba jana zilitunukiwa tuzo iitwayo Humanitarian Award na Taasisi ya Professor Jay kutambua mchango wao katika kusaidia jamii.
Tangu ianzishwe mwaka 2023, Taasisi ya Professor Jay imetoa misaada ya matibabu na pia elimu ya afya kwa wagonjwa wengi hususani wa figo.
Pamoja na Simba na Yanga kupata tuzo hizo pia mjumbe wa zamani wa Bodi ya Simba, Professor Mohammed Janabi nae alitunukiwa tuzo kwenye hafla hiyo.