Simba yapokea mwaliko wa APR kutoka Rwanda
Sisti Herman
July 17, 2025
Share :
Klabu ya Simba imeripotiwa kupokea mwaliko kutoka nchini Rwanda wa klabu ya APR kucheza mechi ya kirafiki.
APR ambayo itaiwakilisha Rwanda kwenye michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) msimu ujao, imeomba kujipima na Simba katika mchezo ambao umepangwa kupigwa kati ya August 1 na August 03
Bado Simba haijathibitisha kushiriki mchezo huo kwani itategemea na mipango yake ya Pre-Season
Endapo Simba itaweka kambi yake ya Pre-Season nje ya Tanzania huenda ikashindwa kushiriki mchezo huo katika tarehe iliyopangwa
Kulingana na taarifa za awali, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza maandalizi ya pre-season Julai 25, siku ya Ijumaa.