Simba yashusha mashine ya mabao kutoka Uganda
Sisti Herman
July 2, 2024
Share :
Klabu ya Simba imetangaza kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda, Mukwala Steven Desa kutoka klabu ya Asante Kotoko ya ligi kuu nchini Ghana, ukiwa ni usajili watatu wa klabu hiyo kufanyiwa utambulisho baada ya Lameck Lawi na Joshua Mutale.
Kabla ya kujiunga na Simba, Mukwala amepita kwenye vilabu mbalimbali ikiwemo Asante Kotoko, Vipers na Kampla City zakwao Uganda.
Mukwala amejiunga Simba akiwa na takwimu nzuri za ufungaji katika vilabu alivyopita kama;
- Kampala City Mechi 22, Mabao 13
- Asante Kotoko Mechi 63, Mabao 25
Mukwala amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu.