Simba yashusha mashine ya magoli kutoka Gambia
Sisti Herman
January 15, 2024
Share :
Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kati Pa Omar Jobe raia wa Gambia kutoka FC Zenis ya ligi kuu nchini Kazakhstan.
Kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market mshambuliaji huyo kwa msimu wa 2022/23 pekee amecheza mechi 25 amefunga magoli 13 na kutoa pasi 5 za mabao.