pmbet

Simba yashusha mkata umeme kutoka Nigeria.

Joyce Shedrack

July 6, 2024
Share :

Klabu ya Simba imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa kiungo mkabaji Augustine Okajepha raia wa Nigeria kutoka Rivers United kwa mkataba wa miaka mitatu.
 

Okajepha mwenye umri wa miaka 20 ametambulishwa na wekundu wa msimbazi Simba akiwa ni miongoni mwa wachezaji walionyesha kiwango kikubwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita.

Msimu uliopita alichaguliwa mara mbili katika kikosi bora cha wiki cha michuano ya Kombe la Shirikisho huku kwenye Ligi Kuu ya Nigeria 2023/24 akifanikiwa kufunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mabao matatu, akiibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi mara moja pamoja na kujumuishwa kwenye kikosi bora cha msimu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet